Rasimu ya Katiba [DOWNLOAD]

Baada ya mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya kukamolika, jana Tume ya Katiba ilitoa Rasimu ya Katiba hiyo pale Karimjee Hall, Dar es Salaam.

Unaweza download rasimu hiyo hapa chini na kuacha maoni yako au mtazamo wake juu ya Rasimu hii.

 

DOWNLOAD: Rasimu ya Katiba Mpya (www.tyvavijana.or.tz)

58 Responses to Rasimu ya Katiba [DOWNLOAD]

 1. manase kavishe says:

  shukrani kwa tyva kupata rasimu ya katiba mpya hapa…

 2. mathew marcus glory kutoka iringa says:

  nianze kwa kwa kuwapongeza watanzania kwa kujitahidi kutoa maoni kwa uwazi bila woga pili nizipongeze tume za kukusanya maoni ya katiba kwa kuzunguka nchi nzima na kufanikiwa kupata maoni manzuri ya wananch ambayo yamefanikisha kupata rasimu hii nzuri ambayo nafikiri ndiyo inakwenda kuwa katiba itakayoileta tanzania mpya yenye majibu manzuri kwa watanzania wote lakini nina jambo moja kwa nini baraza la mawaziri likishapendekezwa na rais lipitishwe na wananchi kwa kupigiwa kura na ushindi wao utapimwa kwa kuvuka asilimia 50 muundo wakura uwe ni ndio au hapana watakoshinda wataapishwa moja kwa moja na rais watakaoanguka raisi atateua wengine na hao watthibitishwa na bunge kisha wataapishwa na rais ahsanten

  • Amos S.Mwanga says:

   Somo la uchumi katikaUTEKELEZI ndio uchumi uliotanda Tanzania sasa kama kitengo rasmi cha mifano cha hisabati kwani uchumi huu hutegemea vifaa vya masomo ya Calculus,Linear algebra,Takwimu, Nadharia ya bahati na sayansi ya komputa wajumbe walioko bunge la katiba sio wachumi waliosoma miaka 47 iliyopita wamebobea kwenye aina hii ya UCHUMI KATIKA UTEKELEZI hivi kudai takwimu zilizokusanywa ni za watanzania wote wakati si kweli kuna maeneo wamehojiwa wengi zaidi KIGOMA, KAGERA NA PEMBA halafu idaiwe ni maoni ya watanzania wote NI matusiwajumbe haiingii akilini

 3. buliga says:

  nianze kwa kwa kuwapongeza watanzania kwa kujitahidi kutoa maoni kwa uwazi bila woga pili nizipongeze tume za kukusanya maoni ya katiba kwa kuzunguka nchi nzima – See more at: http://tyvavijana.or.tz/rasimu-ya-katiba-mpya/#sthash.rzoPGUQd.dpuf

 4. waziri says:

  tume imewabagua waislam kutokana na kutokuzungumzia siku ya ijumaa, waislamu tunataka siku hiyo iwe ya mapumziko kisheria,na serikali iitambue.

  • Allen Humbaro says:

   hutakiwi kusema kwamba mmebaguliwa bali utoe maoni yako ili mabadiliko yaweze fanyika ila ukilalama tu haitasaidia

  • juma mtawa says:

   uislam unahitaji watu wafanye kazi labda ungependekeza kazi zifanywe pia jmosi na jpili nyakati za swala/sala turuhusiwe kwenda misikitini/makanisani

 5. Moshi Yudatadei M says:

  Pamoja na shukran zangu za dhati kwa tume nauliza kwann kusiwe na rais mmoja kwa kila uchao mataifa yaungana zaidi kuliko matengano.pia ni gharama kubwa kuwa marais watatu mabaraza matatu ya mawazr nk

 6. Jerremiah Isaack Kilato says:

  RASIMU YA KATIBA

  DIBAJI:

  Maoni haya yamezingatia yafuatayo.
  1) Rasimu hii ya Kamati ya Katiba imejumuisha mawazo ya Watanzania wote kwa usawa, bila kushawishiwa na vikundi au itikadi yoyote iwe ya kisiasa, kidini, kijinsia au kikabila. Kwa kuzingatia hayo maoni haya yanalenga kuboresha uelewa wa Misingi au Nguzo za Katiba.
  2) Maoni haya yanalenga kuitenganisha Katiba Hii na mivutano au ushindani wa wanasiasa na itikadi zao. Tukiweza kuunda Katiba nzuri, ya kuleta amani ya kweli isiyo ya vitisho,woga au unafiki, na yenye kuleta maendeleo kwa Watanzania wote, tutakuwa wote tumeshinda na hakuna aliyeshindwa.
  3) Maoni haya yanataka Katiba ya Jamhuri ya Muungano iwe kitu imara na cha kudumu kwa angalau miaka mingine Hamsini. Tusilazimike kubadilibadili vipengele vyake.

  MAONI MTAMBUKO:

  1. Kazi Nzuri: Turekebishe mawazo kujirudia–rudia, tuepuke details zisizo za lazima na tuzingatie grammar.
  2. Misingi/NGUZO ZA KATIBA
  Nguzo au Misingi ya Katiba iainishwe wazi wazi mwanzo kabisa wa Katiba yenyewe, na iwe na ibara yake mara baada ya utangulizi au katika utangulizi.

  Tuongeze UKWELI katika Misingi ya Katiba.
  Watanzania tumeteswa sana na uongo wa kulaghaniwa na viongozi kwa kutokutuambia ukweli halisi wa kinachotokea. Katiba iseme waziwazi kwamba ni marufuku kwa Mtumishi wa Umma yeyote kusema uongo, au kuficha ukweli kwa maneno ya mzunguko.

  Misingi au Nguzo za Katiba ziwe:
  a/ Utu: Kuheshimu utu wa kila Mtanzania, iwe marufuku kumdharau mtanzania au kumwita Mtanzania mwenzako majina ya kubeza au zarau.
  b/ Uhuru: Marufuku kushurutisha au kulazimisha siasa, sera, imani, na mtazamo wowote. Kila Mtanzania awe na mtazamo wa siasa, sera, imani wa ridhaa yake mwenyewe bila kushurutishwa na chombo, au mtu yeyote mradi msimamo huo haupingani na sheria yoyote iliyoundwa chini ya misingi ya Katiba hii.
  c/ Ukweli: Marufuku kutumia hoja za uongo, kubabaisha. Watanzania
  wasidanganywe na chombo chochote.
  d/ Haki: Mtanzania asinyimwe haki, asibaguliwe na kupuuzwa au kuteswa bure.
  e/ Usawa, Udugu, Umoja na Amani: Iwe marufuku kueneza sera, au siasa za
  chuki, kuwagawa Watanzania, na ubaguzi wa aina yoyote.

  3. Uraia.
  Raia wa Jamhuri ya Tanzania atambuliwe Kikatiba.
  a/ Raia wa Kuzaliwa asiye na mahali pengine popote pa kukimbilia isipokuwa kama mkimbizi atofautishwe na raia wa kujiandikisha, na haki zake zitambulike Kikatiba na zizingatiwe. Ziwe pamoja na:
  – Kupata mahali pa kuishi (ardhi) wasihamishwe-hamishwe ovyo bila maandalizi na mpango sanifu.
  – Kupata Elimu (masomo) Kusomeshwa vizuri, si mradi elimu au kidatu fulani tu, na kwa bei nafuu kama sio bure. Mtanzia aliye elimika ni rasilimali ya taifa.
  – Kupata kazi na mafao yake, na wasioweza kuajiriwa wapewe namna ya kujikimu, pamoja na mafao ya uzeeni.
  – Kupata fursa za kuwekeza na kuanzisha miradi bila kusumbuliwa na mamlaka yoyote.
  b/ Raia wa kuandikishwa: Vigezo vya kumuandiksha mgeni uraia vianishwe Kikatiba. Aidha
  kuishi muda mrefu, kufanya kazi na hata kuwekeza visikubalike, visiwe sababu ya
  kukubaliwa Uraia.
  c/ Ibara inayoelezea uraia iongezwe mara baada ya ibara inayofafanua mipaka, alama, lugha
  utamaduni na Tunu za Taifa.

  4. Hoja zifuatazo zinakubalika pamoja na maelezo nyongeza yaliyoonyeshwa:

  a/ Serikali Tatu:
  Ukweli ni kwamba muungano halisi ni kuwa na Taifa Moja, na Serikali moja.
  Kwa kuwa hilo limeshindikana kwa shinikizo la Zanzibar, basi tuwape Watanganyika nao
  haki sawa na Wanzanzibari kwa kuwa na Serikali yao kamili.
  Serikali ya Muungano itambulike Kikatiba kwamba ndiyo Serikali Kuu ya Taifa la Tanzania
  na Katiba yake iwe msingi wa Katiba Nyongeza za Serikali Shirikishi.

  b/ Mihili ya Utawala Mitatu:
  Bunge, Mahakama na Serikali (Utawala) ibaki kuwa Mihimili yetu ya Utawala, lakini kuwe na vipengele vya kuhakikisha uhuru wa kila Mhimili. Aidha Bunge na Mahakama yasiigope Serikali, yasimuogope Rais na Wizara zake hususan Ulinzi, Polisi, au Usalama wa Taifa, wala wasiwaonee aibu au kujipendekeza kwa mamlaka yoyote katika kutenda haki na kusema ukweli. Aidha sheria zote zitungwe kwa maslahi ya Taifa na zitekelezwe na mahakama kwa kufuata haki, na ukweli bila upendeleo au woga wowote.

  Watendaji wakuu wote wawe na uhuru kamili Kikatiba katika kutekeleza wajibu wao, na hasa wale wanaoteuliwa na Rais, hususani Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Wakuu, Majaji, Msajili wa Mahakama, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Watumishi Wakuu wa Umma, Wakuu wa Ulinzi, Polisi na Usalama wa Taifa, Gavana wa Benki Kuu, Kamishna wa Mapato, Msajili wa Vyama vya Siasa, Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi na Wakuu wengine. Uhuru wao uainishwe kikatiba na kisheria.

  Pia Katiba ianishe vipengele vitakavyo msaidia Rais asipendelee Kabila, Dini, Mwelekeo wa Siasa, Sehemu Mtu anakotoka, au Rangi katika uteuzi wake wa watendaji wakuu. Uteuzi wowote uridhiwe na Bunge.

  c/ Kwa mantiki hiyo, tunaafiki Mawaziri wasitokane na wabunge, wabunge wa viti maalumu au wa kuteuliwa wasiwepo, na mtu (Raia) wa kuzaliwa aruhusiwe kugombea nafasi ya Uraisi, Ubunge na nafasi yoyote nyingine ya utumishi wa umma iwe ya kuteuliwa au ya kuchaguliwa, kama Mgombea Binafsi.
  d/ Chombo Maalum chenye mamlaka ya kumhoji Rais, Mamlaka yoyote ya Serikali, kuhoji Mahakama, kulihoji Bunge na watumishi wa umma kuhusu utekelezaji au ukiukwaji wa vipengele vya Katiba hii, kiundwe na kitambulike Ki-Katiba.

  5. Ufafanuzi zaidi utolewe kwa kwa maneno yafuatayo, pamoja na tofauti zake:
  a/ Raia, Mwananchi, Mtanzania, Mkazi wa Tanzania, Binadamu, na Mtu anayeishi Tanzania. Aidha haki zao nazo ziainishwe hasa zile zinazosimamiwa na Katiba hii, na zile zinazopashwa kutelezwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

  b/ Serikali, Mamlaka ya Nchi, Kiongozi, nazo zifafanuliwe.

  6. Majimbo ya Uchaguzi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yawekewe vigezo sawa, kama ni Mikoa au Wilaya, au hata kama ni idadi ya watu wanaowakilishwa, basi iwe hivyo kwa Tanganyika, (Tanzania Bara) na Zanzibar.

  7. Jina “Tanganyika” litambuliwe na Katiba hii na neno “Tanzania Bara” lisitumike. “Tanzania” iwe ni ufupisho wa “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”.

  8. Serikali isiwe na dini, lakini iheshimu dini na imani za kila Mtanzania bila ubaguzi, woga, au upendeleo, mradi dini hizo hazina vipengele vinavyopingana na masharti ya Katiba hii. Kwa mantiki hiyo kila Mtanzania alazimike kuheshimu dini na imani ya Mtanzania mwingine. Iwe marufuku kwa Mtanzania yeyote kukashifu, kuzarau au kubeza dini au imani ya Mtanzania mwingine. Iwe marufuku kwa Mtanzania kumpachika majina ya dharau Mtanzania mwingine kwa misingi ya dini au imani kama vile mshenzi, kafiri , shetani ……….nakadhalika.

  II MAONI KWA VIPENGELE MBALI MBALI:

  Utangulizi:-
  – Ongeza “Ukweli” kama moja ya misingi inayozingatiwa na kuheshimiwa

  Ibara mbalimbali:

  Ibara ya 2. – Ongeza “Mito na Maziwa”

  Ibara ya 5. – Ongeza “Ukweli”

  Ongeza Ibara mpya itakayofafanua “Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” na imtofautishe “Raia wa kuzaliwa” na “Raia wa kuandikishwa” pia ifafanue haki za kila huyo.
  Ibara Ndogo ieleze tofauti kati ya Raia, Mwananchi, Mkazi, Mtanzania, na Mtu kama maneno hayo yanavyotumika katika katiba hii. Aidha tuepuke kunukuu haki za “MTU” kama zinavyo tambulika katika Katiba ya Umoja wa Mataifa.

  Ibara zifuatazo zisomeke au zirekebishwe ifuatavyo:
  7(2) (c) isomeke “Utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa………………

  7(2) (e) isomeke “Uchumi wa Taifa Unasimamiwa, unapangwa na kukuzwa kwa
  ulinganifu kwa pamoja na kwa namna ambayo unanufaisha wananchi wote.

  7(2)(h) isomeke “Fursa na haki zilizo sawa kwa wananchi wote wanawake na wanaume zinatolewa bila ya kujali rangi, kabila nasaba, dini, au hali ya mtu

  8(8) Isomeke “Katiba hii itakuwa Katiba Mama, na Sheria kuu katika Jamhuri ya Muungano. Kwa mantiki hii, Uundaji wa Katiba za washiriki wa Muungano sasa na baadae Watazingatia masharti ya Katiba hii.

  11-(2) (a) Kisiasa
  (i) Isomeke “Kuhakikisha kuwa hakuna dhulma, vitisho ubaguzi……………………..”
  (b) Kijamii
  (ii) Isomeke “Kuhakikisha kwamba nafasi na fursa zilizo sawa kwa raia wote zinatolewa bila kujali rangi……….., bali kwa kuzingatia uwezo na ujuzi wa mtu.

  11-(2) (c) Kiuchumi: Ondoa details na kujirudia-rudia kwa mawazo. Pia
  ikiwezekana kila ibara ndogo ianzie na kianzio cha
  “Kuhakikisha…….”ili mtiririko ueleweke.

  13-(1) (b) isomeke “Yanamuwajibisha kiongozi…………………..”

  15-(2) (a) Ondoa sehemu ya mwisho ya sentensi kuanzia “isipokuwa……….”

  (b) Haieleweki, Ni lini Mtumishi huyo atakuwa ameshusha hadhi ya utumishi wa umma? Tunashauri ifutwe.

  21-(3) inapuuza uzoefu na dhana ya “Rasilimali watu” na ujuzi wa watu. Maoni yetu ni kwamba watu walioelimishwa kwa gharama ya Taifa, hasa wataalamu kama Maprofesa, Majaji,..etc. waendelee kutumika katika nyadhifa za namna hii na za ushauri, mradi kwamba hawajihusishi na ubinafsi, unafiki, uongo na ufisadi.

  Sura ya NNE izungumzie “MTANZANIA” au “RAIA WA JAMHURI YA MUUNGANO” na sio “BINADAMU” maana sio Binadamu wote wanataka kufuata sera na masharti ya Katiba yetu. Kuna Binadamu ambao wanakumbatia ubaguzi, Udikteta, …..etc.

  Ibara ya 24 – (4) iweke chombo kinachosimamia utekelezaji wa vipengere vya katiba hii, bila kujali mamlaka yoyote.

  27 – (2) Utaratibu wa sheria ya kuhakikisha kuwa haki hizo haziingiliwi na mamlaka
  Yoyote, uainishwe.

  30 – (1) Ukweli katika kutoa habari uainishwe ki-katiba.

  31 – (4) Iondolewe, Ibara ndogo 1,2,3 na 5,6,7 zinajitosheleza

  32 – (6) Isomeke “Ni marufuku kwa Dini na Imani ya dini kutumika kwa namna
  yoyote itakayowagawanya wananchi, kuleta uhasama.

  37: Haki za kijamii za Raia wa Jamhuri ya Muungano ziainshwe kikatiba katika Katiba hii
  na zitofautishwe na zile za raia wa nchi nyingine ambaye labda ni mkazi tu(hataki
  kujiandisha) na pia zitofautishwe na zile za Raia wa kujiandikisha.

  38 – (1) (e) isomeke “Kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa upesi” maana haki
  inayocheleweshwa ni haki iliyokataliwa.

  39 – (1) Yaongezwe maneno “ ikiwa ni pamoja na lishe bora, malazi na mavazi safi,
  pamoja na tiba nzuri.

  42 – (2) Isomeke “Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu utakaohakikisha haki zote
  zinapatikana kwa watoto wote bila ubaguzi wa iana yoyote”

  44 – (2) Iondolewe haiongezi kitu.

  45 – (1) Isomeke “Makundi madogo katika jamii yana haki ya
  (a) Kushiriki
  (b) Kupewa ….

  46 – (1) Iongezewe “kumiliki na kurithi ardhi na mali”

  47 – (d) Isomeke “kulelewa na kupata misaada kutoka kwa mamlaka ya nchi hususani
  matibabu, lishe na malazi, na huduma nyingine bure. Aidha Wazee wapewe
  huduma kwanza kabla ya wengine, na wasilipishwe ushuru au kodi ya iana
  yoyote.

  50 – (5) Isomeke “Kila mtu anao wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli ……………….”

  54 – (1) Isomeke “Mtu ambaye kabla ya Katika hii kuanza kutumika ni raia wa Jamhuri ya
  Muungano, ataendelea kuwa raia kwa kuzaliwa au kuandishwa kama alivyokuwa
  kabla katika hii kuanza kutumika.”

  55 – (1) Isomeke “Kila mtu ambaye ni Tanganyika au Zanzibar atakuwa raia wa Jamhuri……”

  46 – (1) Isomeke “Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii mtu ambaye atakuwa
  mkazi wa Tanganyika au Zanzibar kwa muda usiopungua miaka saba mfululizo, na
  ambaye ametimiza masharti ……..”.

  56 – Iongezewe ibara ndogo inayohusu uraia wa nchi mbili au zaidi. Ibara iridhie au
  ikanushe.

  57 – (1) Iongozwe ibara (d) ndogo inayotamka kwamba “Serikali ya Jamhuri ya
  Muungano wa Tanzania ndiyo serikali kuu.

  57 – (1) – (c) Isomeke “Serikali ya Tanganyika”

  57 – (3) itumie “Serikali ya Tanganyika “ sio “Tanzania Bara”

  62 – (2) iongozewe sharti la “Mradi haiathiri kipengele chochote cha Katiba hii”

  65 – (1) itumie “Serikali ya Tanganyika”

  65 – (2) iondolewe. Uundaji wa serikali za mitaa uwe jukumu la washirika.

  66 – (3) (c) isomeke “Rais wa Tanganyika”

  69 – (1) (a) Mamlaka au chombo maalum kilicho huru kiundwe tofauti na “Ikulu”
  kusimamia “Katiba ya Jamhuri ya Muungano”

  75 – (1) (d) Isomeke “Wakati wa kugombea , ana umri usiopungua miaka arobaini (40)
  na usiozidi miaka themanini (80)|

  75 – (2) Iongezewe “Rushwa au ufisadi”

  76 – Iongezewe ibara ndogo inayo ruhusu Rais mstaafu kugombea tena urais baada ya
  kupumzika kwa walau kwa miaka kumi.

  87 – (3) Iondolewe au kuwe na “Makamu wa Rais”Wawili mmoja kutoka Tanganyika na
  wa pili kutoka Zanzibar.

  93 – (4) Iondolewe. Uteuzi uzingatie ujuzi, uzoefu na weledi tu.

  94 – (1) – (b) Iongezewe “Katika fani husika”

  114 – (5) Iondolewe. Bunge lingoje siku 60.

  117 – (1) Asiwepo mbunge wa kuteuliwa

  131 – (4) Iondolewe. Ama sivyo kuwe na Manaibu Spika wawili, kutoka Tanganyika na
  Zanzibar.

  145 – (1) Isomeke “Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki Mahakama ya Jamhuri ya
  Muungano itazingatia ukweli na itaongozwa na masharti ya Katiba hii……………”

  152 – (2) Ifutwe ama sivyo kuwe na manaibu wawili kutoka kila upande wa Washirika.

  153 – (3) Ifutwe kuepusha upendeleo wa iana yoyote.

  157 – (2) (a) Isomeke “Rais, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu atamsimamisha kazi Jaji
  huyo.

  157 – (3) (c ) Iongezewe “ na kutozingatia ukweli”

  157 – (5) Itoke yote. Vipengele vya vya Katiba visiyumbe.

  162 – (2) Itoke yote. Rais asije akashawishika kupendelea.

  179 – (2) (a) Iongezewe “bila upendeleo, woga au unafiki wowote”:

  213 – (1) Iongezewe kipengele kitakachotaka “Bunge liidhinishe mikopo yote ya Serikali”

  214 – (2) Iongezewe kipengele kitakachotaka “Bunge liidhinishe dhamana hizo”.

  221 – (1) (a) Iongezewe “ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi na Usalama
  wa Taifa”.

  228 – Iongezewe ibara ndogo ya kupiga “Marufuku polisi kuonea, kusingizia,
  kubambikizia kesi na kusema uongo.”

  HITIMISHO

  Tunapenda kuipongeza Kamati ya Katiba kwa kazi nzuri. Tunaitakia usimamizi mzuri wa kazi hii mpaka utimilifu wake. Tunajua kuwa itapata upinzani katika vipengele kadhaa hasa kutoka kwa wale waliokuwa wanalindwa na Katiba ya sasa. Tunaomba wasitishwe na hilo, bali walitafsiri kuwa ni changamoto ya mafanikio. Tunaitakia Kamati kila la kheri.

  >>>>>>>>>>>>>>>>>ooOoo<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

 7. sam says:

  hivi kwanini tusifanye kama Kenya, hao mabalozi na mawaziri wa kuchaguana kwa kujuana wanakua wazembe,watangaze kazi, tuombe, tufanyiwe interview nchi iende mbele.

  sio mtu ni mtaalamu wa uchumi achaguliwe kua waziri wa afya!!!&^((&^)(*&

 8. Divine maguge says:

  Natoa pongezi kwa mh Joseph sinde warioba na jopo lake kwa kufanikisha kazi hiyo ngumu, na yenye mzigo wa kuilinda na kuiongoza tanzania inayoendelea.

  Ila nina HOJA au MAONI; KATIKA SURA YA 4 SEHEMU YA KWANZA panasomeka hivi;

  SURA YA NNE
  HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI
  SEHEMU YA KWANZA
  HAKI ZA BINADAMU
  22. Uhuru, utu na usawa wa binadamu
  23. Haki ya kuwa hai
  24. Marufuku kuhusu ubaguzi
  25. Haki ya kutokuwa mtumwa
  26. Uhuru wa mtu binafsi
  27. Haki ya faragha na usalama wa mtu
  28. Uhuru wa mtu kwenda anakotaka
  29. Uhuru wa maoni
  30. Uhuru wa habari na vyombo vya habari
  31. Uhuru wa imani ya dini
  32. Uhuru wa watu kujumuika na kushirikiana na wengine
  33. Uhuru wa kushiriki shughuli za umma
  34. Haki ya kufanya kazi
  35. Haki za wafanyakazi na waajiri
  36. Haki ya kumiliki mali
  37. Haki ya uraia
  38. Haki ya mtuhumiwa na mfungwa
  39. Haki ya watu walio chini ya ulinzi
  40. Uhuru na haki ya mazingira safi na salama
  41. Haki ya elimu na kujifunza
  42. Haki ya mtoto
  43. Haki na wajibu wa vijana
  44. Haki za watu wenye ulemavu
  45. Haki za makundi madogo katika jamii
  46. Haki za wanawake
  47. Haki za waze

  Kwa kuwa katiba ni chombo kitakachodumu, na kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, na kwa kuwa hakuna mtu anaeisemea katiba maana katiba ndiyo itakayowalinda watu wote jasiri na hata wanyonge “KIONGEZWE KIFUNGU CHA 48 HAKI ZA WANAUME” ili isijetokea ikaonekana wao hawana haki maana hazijazungumzwa na katiba, “kwa kuzingatia kwamba mwanaume siyo katiba.

 9. gregory mhamela says:

  Mapendekezo kuhusu uboreshaji rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

  Gregory Mhamela
  mhamela4775@yahoo.com

  Mimi siyo mjuvi wala mtaalamu wa masuala ya ukatiba lakini ninaomba kuwasilisha maoni yangu binafsi kwa minajili ya kuifanya rasimu iwe bora zaidi baada ya kuisoma rasimu hiyo kwenye ‘Nipashe’ ya Juni 10, 2013, ambayo sina hakika kama ni timilifu kama ilivyo kwenye kabrasha kubwa ‘original’.

  1. Kupangilia upya mtiririko na muundo wa vichwa vya habari na maudhui
  Kwa kuwa nchi iko kwenye mchakato wa kutunga katiba mpya inafaa pia hata mpangilio wa mtiririko na muundo wa vichwa vyake vikuu na vidogo vya habari ukarekebishwa ili kudhihirisha ‘upya’ wake na ubunifu ulitumika katika uundaji na uandishi – hasa kuifanya iwe katiba rafiki. Ukitazama kwa makini sana muundo na mtiriko wa rasimu ya katiba ulivyo hivi sasa utaona kuwa mtiririko na muundo wa maudhui haitofautia nasa na ule wa katiba ya mwaka 1977. Pia rasimu ina marudio ya kauli (statement) na masuala – yaani kauli moja katika sehemu moja unaikuta imerudiwa kuandikwa katika sehemu moja nyingine au sehemu kadhaa nyingine.

  1.1. Kuingiza kipengele cha ‘historia’
  Sina uhakika sana kuhusu aina ya kichwa cha habari cha kipengele hiki. Kinaweza kuwa:

  Historia ya katiba za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  Maudhui yake yatalenga kuelezea idadi ya katiba za Jamhuri na marekebisho yake kwa tarehe; au, kama ilivyofanya gazeti la Mwananchi toleo la Agosti 11, 2013 katika makala iliyoandikwa na Dismas Lyassa (Hongera!) kwenye aya zilizo chini ya kichwa cha habai ‘Ilikoanzia katiba’. Hata hivyo ‘nyama’ nyingi zaidi kidogo inahitaji kuongezwa kila mwaka wa tukio la katiba ili kunogesha uelewa wa mtiririko wa matukio hayo.

  Historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  Maudhui yake yatalenga kuelezea chimbuko la jamhuri, katiba ya kwanza na jinsi ilivyokuwa inarekebishwa na hasa mambo/masuala yaliyopelekea kufikia hatua ya kuamua kutunga hii katiba mpya. Ikiwa hili litakubalika ndipo kifuate kichwa cha habari cha ‘utambulisho wa katiba’ – ‘preamble;

  1.2. Kuingiza kipengele cha utambulisho (preamble)
  Kipengele cha utambulisho (preamble) ni tamko (kauli) la awali kinachoainisha ‘buku’ la katiba ni nini. Hivyo, badala ya Seheme ya Kwanza kuitwa …‘mipaka, alama, utamaduni na tunu za taifa’ …kwenye kichwa cha habari ‘Jamhuri ya Muungano’ kingeitwa ‘Utambulisho wa Katiba’; mathalani:

  Katiba ya Jamhuri ya Muungano

  Utambulisho wa Katiba
  Katiba hii mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa sheria kuu (mama) ya nchi washirika wa muungano ambayo ina sehemu (vipengele, vifungu) (idadi) vya makubaliano ya shirikisho la kidemokrasia linalofuata na kuzingatia mfumo wa vyama vingi vya siasa yaliyopitishwa rasmi na Bunge la Pamoja la Katiba kuhusu uwapo wa serikali tatu zinazotangamana; yaani: 1) Serikali ya [watu wa] ya nchi ya Zanzibar; Serikali ya [watu wa] ya nchi ya Tanganyika, na Serikali ya [watu wa] Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; ambayo inaweka misingi ya haki na usawa binadamu, mgawanyo wa mamlaka mbalimbali za utawala, uongozi, usimamiaji na udhibitiwaji wa serikali kuu na serikali za kila nchi, bunge kuu na mabunge ya kila nchi, muafaka katika masharti ya uteuzi wa tume huru ya uchaguzi, mgombea wa nafasi ya urais wa jamhuri, uwaziri wa jamhuri, ubunge/ uwakilishi wa jamhuri, tawala za mikoa na serikali za mitaa, ukomo wa kuwa madarakani; tija, mapato na matumizi ya fedha na raslimali mbalimbali za jamhuri, mahakama za jamhuri, mahakama za kila nchi na maudhui ya ushirikiano na muungano baina ya nchi na nchi; tume mbalimbali na jinsi katiba hii itakavyokuwa inaweza kurekebishwa/kubadilishwa na kupitishwa.

  Dhamira ya katiba
  (Ninapendekeza kuwa) ile ya tano kuanzia (a) hadi (h) kwenye ‘nyongeza- utangulizi’ ihamishiwe hapa ambapo inafiti vizuri kabisa – ni mahali pake hasa

  Mtu yeyote, chombo, taasisi, jumuiya na wakala wowote wa mamlaka ya nchi na mamlaka ya kila nchi washirika wa jamhuri ya muungano na mamlaka binafsi zitakuwa na wajibu wa kuzingatia na kuyatii masharti ya katiba hii; hivyo, sheria yoyote, mila, desturi au uamuzi wowote wa chombo, ofisa wa serikali na mtu binafsi sharti vifuate na kuendana na masharti[maelekezo/maagizo] yaliyomo kwenye katiba hii na kwamba sheria, kanuni au uamuzi wowote ambao utatungwa na kutolewa ambao hautawiana au hautatangamana na masharti ya katiba hii yatakuwa batili.

  Aidha katiba hii inaweka masharti/maelekezo/maagizo (sijui utofauti wa maneno haya) kuhusu eneo la Jamhuri ya Muungano, tunu za taifa, mamlaka ya wananchi, utii wa katiba, utekelezaji wa malengo ya taifa, misingi na mwelekeo wa sera na shughuli za serikali, maadili na miiko ya uongozi na utumishi wa umma, haki za binadamu, uraia na wajibu wa raia, mamlaka ya jamhuri ya muungano.

  Hivyo, mamlaka na umiliki wa utungaji na ulindaji wa katiba hii ni ya watu wa Jamhuri ya Tanzania ili kujenga na kuimarisha ushirikiano bora zaidi wa muungano, kuimarisha na kulinda haki na uhuru sawa, utulivu na amani, ulinzi, manufaa, maendeleo na ustawi wa pamoja kwa watu wote wa jamhuri kwa njia ya kujitegemea

  Mambo/masuala ya Muungano/shirikisho
  Hivyo basi, mambo na masuala mahsusi ya muungano/shirikisho yatakayokuwa yanashughulikiwa na katiba hii yatakuwa (kama yalivyoorodheshwa katika katiba ya 1997)
  • Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
  o Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano.
  o Madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
  • Uraia na uhamiaji.
  • Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano
  • Ulinzi, usalama, na majeshi.
  • Mambo yanayohusika na hali ya hatari.
  • Mambo ya nchi za nje na mikopo na baiashara ya nchi za nje.
  • Deni la kitaifa
  • Sarafu na fedha
  • Bandari na usafiri wa anga
  • Posta na simu.
  • Kodi ya mapato, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa wa kitaifa
  • Fedha za kigeni.
  • Viwanda na takwimu.
  • Elimu na Baraza la Taifa la mitihani
  o Sayansi, ufundi na teknolojia
  • Maliasili
  • Usafiri na usafirishaji wa anga.
  • Hali ya hewa.
  • Idadi ya watu na takwimu.
  • Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
  • Vyama vya siasa
  o Uchaguzi na upigaji kura
  • Mambo ambayo mabadiliko yake yanahitaji kuungwa mkono na wabunge wa Tanganyika na wabunge wa Zanzibar.
  • Mabunge
  • Wakala wa uchunguzaji makosa ya jinai
  • Magonjwa ya mlipuko na uambukizaji
  • Mikataba, uridhiaji wa tenda na zabuni za kimataifa
  • Kero za Muungano

  1.3. Kuongeza kichwa cha habari cha ‘mambo yasiyokuwa ya muungano/shirikisho’ na maudhui yake

  1.4. Kuhamisha na kubadilisha kichwa cha habari cha ‘nyongeza’ – ‘utangulizi’
  Iwapo mapendekezo hapo juu ya kuingiza dhana ya ‘preamble’ yatakubalika ingefaa kichwa hicho cha habari kifutwe na maudhui yake yote yanayoanzia ‘kwa kuwa sisi…’ na kuhamishiwa kutoka hapo kilipo (kinaning’inia) na kuwekwa chini ya kichwa cha habari cha ‘preamble’ kwa kuwa maudhui ya kipengele hiki ndiyo hasa yanayoweka na kungarisha msingi mkuu wa umiliki wa watu wa katiba mpya.

  Aidha kutokana na kwamba muungano unahusisha ufafanuzi wa ushirikiano wa nchi mbili zenye mamlaka yake kamili kila moja, ingefaa basi angalau kauli ya kwanza ikasomeka:
  ‘Kwa kuwa sisi watu wa nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga [kudumisha na kuendeleza]serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…

  Halafu, kutokana na kwamba eneo hili ni tamko la kusudio pengine ingefaa kauli zinazoambata na kauli za ‘kwa kuwa..’ zikapunguzwa ili zisimchepue msomaji; zibaki chache tu. Kauli nyingine zingweza kuhamishiwa kwenye kichwa cha habari cha ‘utambulisho wa katiba’

  Ikiwa hii inakubalika, basi kauli ya hitimisho la eneo hili lingeweza kurekebishwa na kusomeka; mathalani:

  ‘Hivyo basi, sisi watu wa nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika tunaafiki uwapo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – ambayo ni sovereign nation state – ili kuunda shirikisho bora zaidi, kuimarisha na kudumisha haki, utulivu, uhuru binafsi wa kila mtu, ulinzi wa pamoja, demokrasia na utawala/manejimenti bora kwa misingi wa kila upande kujitegemea na kutegemeana; nchi isiyokuwa na dini; isipokuwa wananchi watakuwa huru kufuata au kutofuata dini yoyote.’

  1.5. Kuingiza kipengele cha ‘maudhui’
  Licha ya kwamba rasimu ina orodha ya muhtasari wa ‘sehemu’ na vifungu vyake vikuu na vidogo ni uandishi mzuri kuichanganua katiba kwa maelezo mafupi; kama vile
  ‘Katiba hii imegawanywa/imegawanyika katika…’
  ‘Sehemu ya kwanza inahusu/inaweka masharti kuhusu/inaelekeza kuwa…’
  ‘Sehemu ya pili…na kadhalika…’

  1.6. Kuhamisha kipengele cha ‘ufafanuzi’ na kuongeza istilahi
  Kipengele hiki kimo kwenye ‘sehemu ya kumi na sita’ chenye kichwa cha habari ‘mengineyo,. Kutokana na kwamba mtu angetaka kujua mapema maana ya maneno yaliyotumika katika katiba hii ingefaa kichwa cha habari hicho kikahamishwa huko kilipo na kuwekwa baada ya kichwa cha habari cha ‘maudhui’ kilichopo hapo juu. Aidha kwa kuwa katiba hii mpya inasuhu dhana mpya ya muungano na shirikisho ingefaa ziingizwe au ziongezwe istilahi za dhana hizo ndio zitolewe fafanuzi wa kina zaidi wa kisheria ili kuzuia mikanganyiko, kero na kuhitalafiana hapo baadaye.

  Aidha ingawa rasimu ya katiba mpya pia inaeleza maudhui yanayotakiwa katika kila ’sehemu’ ingefaa baadhi ya maneno/istilahi zake zikahamishwa na kuwekwa chni ya kichwa cha habari cha ‘ufafanuzi’ na zikatolewa fasiri isio na shaka kisheria badala ya kuyachukulia kimazoea; Mathalani: (istilahi nyingine zimefafanuliwa tayari katika katiba ya 1977 ila inabidi zirekebishwe ili ziendane na mahitaji ya katiba mpya)

  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake….
  Eneo la Jamhuri ya ya Muungano maana yake…
  Shirikisho manna yake….
  Tunu za taifa maana yake…
  Jamhuri ya [nchi ya] Zanzibar maana yake….
  Eneo la Jamhuri ya Zanzibar maana yake…
  Jamhuri ya [nchi ya] Tanganyika maana yake….
  Eneo la nchi ya Tanganyika maana yake…
  Mambo/masuala ya muungano/shirikisho maana yake…
  Mamlaka ya nchi maana yake…
  Mamlaka ya wananchi maana yake…
  Utii wa katiba maana yake maana yake…
  Malengo ya kitaifa [Muungano/shirikisho] maana yake…
  Sera kuhusu mambo ya Muungano/shirikisho maana yake…
  Maadili na miiko ya uongozi na utumishi maana yake…
  Mgongano wa kimasilahi maana yake…
  Marufuku badhi ya vitendo maana yake…
  Haki za binadamu maana yake…
  Haki za Jamhuri ya Zanzibar maana yake…
  Haki za Jamhuri ya Tanganyika maana yake…
  Wajibu wa raia maana yake…
  Uraia maana yake…
  Vyombo vya utendaji vya Jamhuri ya Muungano maana yake…
  Waziri mkazi maana yake…
  Rais wa Jamhuri ya Tanzania maana yake…
  Rais wa Jamhuri ya Zanzibar maana yake…
  Rais wa Jamhuri ya Tanganyika maana yake…
  Baraza la mawaziri la serikali ya Jamhuri ya Tanzania maana yake…
  Baraza la mawaziri la serikali ya Jamhuri ya Tanganyika maana yake…
  Baraza la wawakilishi/mawaziri la serikali ya Jamhuri ya Zanzibar maana yake…
  Uratibu wa mahusiano ya washirika wa Muungano maana yake…
  Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake…
  Hali ya muungano (state of the union) maana yake…
  Ufisadi maana yake…
  Ugaidi maana yake…
  Hati za muungano/shirikisho maana yake…

  2. Uwekaji vichwa vipya vya habari na maudhui yake
  Licha ya kuwa na vichwa vya habari vinavyoitwa ‘sehemu’ ingefaa pia kukawepo na vichwa vya habari vya:

  • Hati za muungano/shirikisho ‘articles of confederation’ au ‘articles of union’ pamoja na ufafanuzi wa istilahi hii na maudhui yake hasa wajibu wa kila mshirika kwenye serikali yake na serikali ya muungano

  • Mipaka ya mamlaka na madaraka ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

  • Majina ya viongozi wakuu wa serikali ya Zanzibar; serikali ya Tanganyika; na serikali ya muungano/shirikisho

 10. isack says:

  kiukweli rasimu imekaa vzr sana ttz wapo baadhiya watu kwa kutaka kujilinda wanaiona haifai na kuanza kuiponda hyo ndo katiba itakamkomboa mtanzania.kuhusu maraisi watatu ni sahihi kabisa kuwa na maraisi watatu ili kulinda muuungano na kuepusha malalamiko kutoka upande mmja wa muungano

 11. Jessica says:

  Swala la uraia wa nchi mbili ungeongezwa kwenye rasimu.

 12. riziki mvungi says:

  katiba yetu tunataka iwe inampa kila mtanzania haki ya kujitawala bila ya kuvunja sheria zilizo wekwa.

 13. riziki mvungi says:

  kiwepo kipengele kinacho wanyima viongozi kuwa na mamlaka makubwa katika uongozi wao.

 14. ni kweli katiba imefanyiwa marekebisho

 15. tume ya mabadiliko ya katiba says:

  Mi sikubari serikali tatu, napinga vikali mno. Hali zetu duni sana, tunaongeza serikali nyingine mbili bado shida.

 16. Florian maro says:

  kwa mimi naona tume ya warioba imefanya kile ambacho watanzania waliwatuma . Tuheshimu mawazo yao

  • kombe says:

   free election board ambayo itatoa haki kwa vyama vyote vya siasa hususani kwa wagombea binafsi ili mradi tu wakubalike na wananchi.

   • Jodre kombe says:

    kikomo cha watoto wa viongozi kupewa kipao mbele kwenye uongozi wakati tumesoma nao sambamba na hakuna geni wanalolijua kutushinda,watoto wa wakulima na wafanyakazi wapewe nafasi za kuongoza taifa kukataa misingi ya rushwa na ufisadi.
    sayasi na technojia ipewe kipao mbele hebu angalia vijana walivyoweka computer nje kariakoo wanauna lock simu,kufanya vitu mbalimbali,aibu kwa nchi kama Rwanda kutushinda kwa kuwekeza katika vituo vya sayansi wakati sisi tupo na nchi kubwa yenye rasilimali za kutosha,hatuwezi hii ni aibu wa kukosa viongozi wenye utashi na vijana,na kuondoa ubinafsi.

 17. simon msuya says:

  katiba hii iwe na manufaa kwa watanzania wote kutoka matabaka yote wawe matajiri au maskin na kutokana na rasimu hii tunaamin tutapata katiba nzuri isiyowapendelea watawala au wapinzani ,kutokana na rasim hii tunaamin rasilimali za Tanzania ziwanufaishe watu wa nchi hii ambayo wao wanasema kuna amani lakin
  si ioni aman hiyo kwa sababu matabaka yanazid kuongezeka masikin wanazid kuwa kuwa maskin na matajir wanazid kuwa matajir ;mungu ibarik tz mungu tubarik wa tz

 18. juma mtawa says:

  Rasimu ya pili ya katiba yetu pamoja na mambo mengi mazuri bado haijaikonga nafsi yangu mimi naona kukosa falsafa ya Taifa kutaifanya katiba iwe kama mwanasesele tutaendelea kuachana na falsafa ya “UDUGU NA KUJITEGEMEA” ambayo inamafungamano makubwa na UJAMAA na kuendelea kuburuzwa na UBEPARI ambao ndio ulioteka kila nyanja ya maisha kwa sasa, hivyo nivema kama jopo la wasomi wazalendo wa medali za siasa,uchumi,jamii na falsafa wangekaa na kutupa dira ambayo ndio ingekua moyo wa katiba (FALSAFA) itakayotuwezesha kuishi na mfumo wa kibepari wenye asili ya kimagharibi bila kuathili mila na desturi zetu kwani hakuna nchi iliyoendelea duniani kupitia tamaduni za kigeni.

 19. Masanja Nzumbi says:

  Nionavyo, Tume ya Jaji Walioba imefanya kazi yake vizuri kwa uadilifu na ueledi mkubwa.Ama kwa hakika wanastahili pongezi nyingi kwani wamezingatia mawazo ya wananchi bila kuathiriwa na ‘Uvyama’. Naamini kuwa watu hawa wanayo hofu ya Mwenye-Enzi Mungu. Hata hivyo kuna watu wana mawazo ‘mgando’, na kila kukicha wanawaza yale yale. Hawawezi kutumia uelewa wao kutokana na elimu zao. Nionavyo mimi, ili tupate Katiba inayotufaa, wabunge wazingatie maoni ya wananchi. ‘Wasichakachue’ kwa ushabiki tu wa vyama- Wasome alama za Nyakati!

  • DOTTO NZUMBI says:

   Hakika viongozi kuweni na huruma kwa kizazi cha Tanzania kwa miaka 50 au zaidi ijayo kwani mtachakachua rasimu ya jaji Warioba kwa manufaa ya wachache lakini hata kama hamtakuwepo duniani adhabu yenu yaja hata katika makazi yenu ya milele maana kizazi cha mtanzania mtakuwa mmekitesa kwa miaka zaidi ya 50 sababu ya kupitisha katiba isiyo na tija kwa mtanzania. Huruma ya Mungu iwaguse mkumbuke kuwa mtakufa na mtahitaji makazi ya milele na amani huko mbinguni je mtayapateje ikiwa umma wa mtanzania mnaufanyia KUFURU KATIKA MAONI YA WANANCHI KUPITIA RASIMU YA WARIOBA?

 20. sulatan says:

  Kwanza tunashkuru wote waliosimamia hili
  Kwenye rasimu ya katiba mpya hii bado haijaridhisha kwenye maswala ya muungano kuwa bunge la jamuhuri ya muungano wa tanzania kupewa asilimia 50 na zanzibar kupewa 20 hapa bado haipa sawa kimaamuzi inaonesha wazi kuwa maamuzi yote yataamuliwa na wabunge wa tanganyika hata kama wabunge wa zanzibar hawatakubali.

 21. said ibrahim says:

  Mbona hii katiba mpya imalenga sana mambo ya uongozi tu na muungana bila kumjadili mwananchi wa hali ya chini inamkwamuaje ktk limbi la umasikini mali asili zetu zinatunufaisheje mwananch walemavu wangozi na viungo ambo hawawezi kufanya kazi katiba mpya inasemaje kuhusu watu hao watoto wa mitaani katiba inasemaje wasaidiwe vipi isiangalie sana mambo ya uongozi tu iangalie na mwananchi wa tz ambao ndiyo wenye katiba inawasaidi nn katba mpya msiangalie uongozitu

 22. MSESE JR says:

  NAIPONGEZA SANA TUME YA KATIBA KWA KAZI SAFI SANA,OMBI LANGU NI KWA NDG ZANGU WATAKAOBAHATIKA KUUNDA BUNGE LA KATIBA WATANGULIZE UTAIFA MBELE KWANI KTK HILI TUACHE KABISAA USWAHILI,MUNGU IBARIKI TANZANIA Amina.

 23. NICE says:

  katiba ifafanue adhabu juu ya mwanaume kuhusu ukatili wanaoufanya juu ya kutelekeza familia zao na kukataa mimba, kwani wanamnyima mtoto haki yake.

 24. Elisamehe Z. Yohana says:

  Pamoja na pongezi najiuliza kama serkali itabadilika na kutii kielelezo cha ardhi ni mali ya watanzania ni urisi wa viizazi hata vizazl maana ni ajabu mgeni kupewa eneo ni vgumu kumnyang’anya

 25. MIMI BINAFSI NAYAKUBALI MABADILIKO YA KATIBA, ISPOKUWA VIPENGELE VIFUATAVYO; 1.BADALA YA KUITWA TANZANIA BARA, IITWE TANGANYIKA, KUHU MIHIMILI MITATU YAANI SERIKALI, BUNGE NA MAHAKAMA, MIHIMILI HIYO IWE HURU ISIINGILIANE, AIDHA RAIS AWE NA MIPAKA PIA AWE NA MAAMUZI YA MWISHO JUU YA MIHIMILI HIYO KUPITIA CHOMBO MAALUMU KAMA TUME PALE INAPOTOKEA MGONGANO WA KIMASLAHI,KUHUSU WAKUU WA WILAYA, MIKOA, A/TARAFA WACHAGULIWE NA WANANCHI WENYEWE, MAWAZIRI WAWE WAKUAJIRIWA NA TUME YA AJIRA KAMA AJIRA ZINGINE, LA MWISHO AJIRA ZA WATUMISHI WA UMMA ZIRUDISHWE NGAZI YA HALMASHURI KWA TUME YA AJIRA KWENDA KUSIMAMIA ZOEZI HILO NA KUZINGATIA VIGEZO.

 26. Elisamehe Z. Yohana says:

  Tuwe wazalendo waaminifu ktk nafasi zetu hii katiba itakua safii; pasipo uaminifu bomu; maana mtumishi wa uma anapotiliwa mashaka ya utumishi wake asmamishwe kazi afanyiwe uchunguz bila yeye kushirikishwa asiharibu ushahidi. Mtumishi wa uma hapaswi kuvunja au kukiuka mashartii ya katiba. Inaumiza kiongozi mtuhumiwa kutopelekwa mahakamani mapema baada ya kubainika ana kosa. Rejea kipengere cha miiko ya uongozi wa uma.

 27. Prinse Tomcy says:

  Prinse Tomcy mkopo wa fedha Company Inc

  Sisi kutoa mikopo kwa watu binafsi , vikundi au makampuni:
  Inawezekana kupata mkopo kwa kiasi cha $ 5,000.00 na hadi $ 100,000,000.00 kutoka kampuni yetu ( Prinse Tomcy mkopo wa fedha COMPANY INC ). Sisi kutoa mikopo kwa mtu binafsi na kampuni kwa kiwango cha riba ya 2% ya udhamini (ID , kijamii usalama, kuwa 100% ).
  Kama wewe ni miaka 18 na zaidi, na una kazi na akaunti kazi benki , basi ni haki kwa ajili ya mkopo wa fedha bila kuchelewa na ndani ya 2 hadi 3 ya biashara days.We kutoa mkopo binafsi, biashara mkopo, mikopo, mkopo wa gari, mkopo elimu, usafiri na burudani mkopo. Aidha, sisi kutoa mikopo katika fomu ofUnsecured mkopo, kupata mkopo, Bad mikopo na uimarishaji wa madeni ya mikopo.
  Tu kutuma e-mail: prinsetomcy@yahoo.com

  Kama kuandika nyuma kama una nia, tafadhali kujaza fomu hii ili tuweze kuanza mikopo usindikaji
  Wakopaji na utekelezaji wa taarifa kamili
  Majina ya waombaji : ____________________
  Kiasi mkopo ombi : __________________
  Urefu wa Loan: _________________
  Madhumuni ya mkopo : _______________________
  Anwani ya mwombaji : _________________
  Kazi: __________________________
  City: ___________________________
  Nchi : __________________________
  Nchi : __________________________
  Ghana : _____________________
  Umri: ________________________
  Simu: ___________________________________

  Tunatarajia kwamba uhusiano mzuri kati ya wewe na mkopo huduma Prinse Tomcy

  Prinse Tomcy firma Financiera de préstamos , Inc
  Contacto : E -mail: prinsetomcy@yahoo.com
  C. E.O.Prinse Tomcy
  mkurugenzi

 28. hindu healings says:

  INDIAN UPONYAJI khaki KIHINDU )
  Ongea Marekani msaada wa kiroho aina yoyote ya
  Matatizo kama vile .

  [1] Kuangalia kwa ajili ya matunda ya tumbo .
  [2] Power kufanikiwa katika biashara .
  [3] Chanzo cha wanaomiliki high nafasi katika ofisi .
  [4] Chanzo cha kushinda bahati nasibu.
  [5] na uwezo wa kupata kazi nzuri.
  [6 ] Chanzo kiroho kupata utajiri bila ya mauaji .
  [7 ] Chanzo haraka kupata kukuza katika ofisi .
  [8] mali kimya.
  [9] Business Boeing.
  [10] Chanzo cha kupata mkataba wa kazi.
  [11] pete ya dhahabu kwa ajili ya ulinzi .
  [12] asili ya afya .
  [13] Instant kibali visa.
  [14 ] Upendo pete .
  [15] Epuka alionyesha katika ndoa .
  [16] Chanzo cha kushinda na uhalifu wowote katika jamii.
  [17] Chanzo cha kupata kutibiwa ya maradhi yoyote.
  [18] ndoto mbaya .
  [19] na uwezo wa kufanya mwanamke .
  [20] jeshi tone.
  [21] kile ninachosema.
  [22] Gonga kutoweka.
  [23 ] No ahadi zaidi na kushindwa.
  [24] mafanikio ya mtihani.
  [25] Power ujumla lengo katika maisha .
  [26] Power kuacha kufanya ngono katika ndoto.
  (27 ) Habari Lucky
  Kuwasiliana nasi: hindu.healings @ yahoo.com
  (+234 7013638582) – (+234 8186183200)

 29. JAMES ANN says:

  Je, unahitaji mkopo? Kulipa bili na madeni ? Wasiliana nasi kwa jina lako, posta, tarehe ya kumalizika muda , namba ya simu , kazi , madhumuni ya mkopo , sakafu , wewe kutumika kabla ya ?
  JAMES ANN sahihi ya fedha mkopo, Inc
  Maelezo ya kuwasiliana : Barua pepe: jamesannbb@yahoo.com
  C E O JAMES ANN
  directo

  JAMES ANN mkopo wa fedha Company Inc

  Sisi kutoa mikopo kwa watu binafsi , vikundi au makampuni:
  Inawezekana kupata mkopo kwa kiasi cha $ 5,000.00 na hadi $ 18,000,000.00 kutoka kampuni yetu (JAMES ANN mkopo wa fedha COMPANY INC ).
  Sisi kutoa mikopo kwa mtu binafsi na kampuni kwa kiwango cha riba ya 2% ya udhamini (ID , usalama wa kijamii , kuwa 100%).
  Kama wewe ni miaka 18 na zaidi, na una kazi na akaunti kazi benki , basi ni haki kwa ajili ya mkopo wa fedha bila kuchelewa na ndani ya 2 hadi 3 ya siku biashara.
  Sisi kutoa mkopo binafsi , biashara mkopo, mikopo, mkopo wa gari , elimu mkopo, kusafiri na burudani mkopo. Aidha, sisi kutoa mikopo katika fomu ya
  Unsecured mkopo, kupata mkopo, Bad mikopo na uimarishaji wa madeni ya mikopo.
  Tu kutuma e-mail: jamesannbb@yahoo.com

 30. Kilavo Mlaki says:

  IWAPO HAKUNA MAAMUZI YATAKAYOFANYIKA KWENYE UUNDWAJI WA KATIBA KUTOKANA NA AKIDI KUTOKURUHUSU BUNGE LIVUNJWE KUPUNGUZA GHARAMA

 31. Emmanuel Phenias says:

  Mungu asimame katka mchakato mzima wa uundaj wa katib mpya.p

 32. maurice finance says:

  hello,
  Mimi nina Mr Maurice kuthibitishwa, reputable, halali & vibali fedha Taasisi. Mimi mkopo fedha nje kwa watu wanaohitaji msaada wa kifedha. Je, una mikopo mbaya au wewe ni katika haja ya fedha ya kulipa madeni? Nataka kutumia kati ya kuwajulisha kuwa sisi kutoa kuaminika msaada walengwa kama sisi itakuwa njema kwa kutoa mkopo. Huduma zinazotolewa. Wasiliana na email: mauricefinance@hotmail.com
  ni pamoja na:

  refinance
  Home Loan
  mikopo
  Home Improvement
  mwanafunzi mkopo
  mvumbuzi Loan
  mkopo wa gari
  Hard fedha mkopo
  madeni Consolidation
  Mstari wa mikopo
  Business Loan
  mkopo binafsi
  Mikopo ya kimataifa

  Kuwasiliana nasi leo na kuruhusu sisi kukusaidia nje ya fedha hardship.Send sisi e-mail na ombi kwa maombi ya mkopo kujaza-up. no
  usalama ya kijamii required na hakuna hundi mikopo inahitajika. Kupokea fedha katika chini ya masaa 24. 100% idhini uhakika.

  Wasiliana na email: mauricefinance@hotmail.com

  Regards,
  Mr Maurice.

 33. Epa Sanga says:

  Rasimu imekaa vyema ndiyo maana ccm wanaiogopa lakini wakiingiza maono yao binafsi tutaipigia kura ya hapana. MUNGU IBARIKI TANZANIA

 34. Amir says:

  Kila mtanzania anasitaili kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wake,apo ni sawa. Ninakwazika
  inaposomeka kuwa kila mtu anasitaili kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wake.
  Kama rais wa Tanzania uchaguliwa midemokrasia na watanzania,sasa
  , iwe vipi Rais huyo awe ni wa kila mtu….kama isemavyo katiba na ndo kiapo chake cha kiofisi? Kwasababu katiba ndivyo imuagizavyo. Binafsi nakwazika
  na sheria hiyo inawanyoya watanzania. Asante.

 35. Nawashukuru wote walioshiriki kututengenezea katiba bora ya baadae ambayo kwayo vizazi vyote vimeshiriki kutoa maoni yao na bila kujali itikadi zetu za aina yoyote ile rasimu hii imezingatia haki,usawa,maslahi,utu, utawala,ushiriki sawa katika maamuzi yote n.k. Me naamini tukiacha ushabiki wa kisiasa, maslai binafsi na mengine hatunabudi kuiunga mkono wa baraka na heri rasimu ili tupate katiba safi na bora.Nawashukuru wote waliojitoa kwa ajili ya taifa hili lenye ndoto nyingi nzuri.Mungu ibariki Tanganyika.Mungu ibariki Tanzania

 36. Zenobi Hoka says:

  Mungu ilinde amani yetu ya watanzania.

 37. Dominic Magadula says:

  Mimi awal ya yote,naishukuru tume ya Warioba.Yamkini kabisa,Rasim ya katiba ikifuatwa bila kupepesa macho,itatimiza haja na kiu ya watanzania mbali na serikali tatu inayo gombaniwa.Pili naomba makundi km vjana,wavuvi,wachimbaj madn wadgowadogo,wakulima na wafugaji,afya/elimu bora zitambulike kkatiba bila ubaguz wowote.

 38. neta netan says:

  kama mumegoma kutengeneza katiba,simuache tu,naona mnamaliza pesa tu.

 39. Hussein Pazi says:

  jamani viongozi naomba tengenezeni katiba mzuri kwa ajili ya wananchi si kwaajili ya maendeo ya nchi

 40. Eric says:

  Sawa mmevunja bunge la katba ila wajumbe wengne hawapo sizani kama itakua baraka sana cha muhum waiten ukawa muyamalize ili rasim iyo ije kwetu wananch ikiwa na baraka za wajumbe wote

 41. Kwanza nawape pole na michakato mliyoifanya name changamoto mlizokutana nazo,pili naomba rasmu hii izingatiwe kama ilivyo pangwa Pasipo kujali high level wala lower.

 42. Mr Ngowi says:

  Katiba kwa sasa tumeipoke kwa mikono yote ingawa kuna vipande ambavyo bado hatujaona vikizungumziwa ,kama wafanyabiasha na niwatu muhimu sana katika kuuinua uchumi wa taifa letu.

 43. We need a good constitution in order to have a good nation for the new generation

 44. amiri simpo says:

  hongera sana mheshimiwa walioba na kamati yake kwa ujumla kwa kutuweka karibu na katiba yetu

 45. DANIFORD AMOS DANDA says:

  MIM KWA MAWAZO YANGU NAFIKILI KWASABABA KATIBA SIKITU KIDOGO KWA TAIFA KWANINI TUSIAHILISHE MASWALA YA KATIBS NAKISHA KUTUMIA KATIBA YA AWALI NAKAMA KUNA MAPUNGUFU AU MAONGEZEKO KTK KATIBA YA ZAMANI BASI KIPENGE HICHO TUNA UWEZO WA KUKITOA AU KUKIOONGEZA KWA KUPITIA KATIBA ILEILE BADALA YA KUIINGIZA SELIKALI HASALA !

 46. jofrey mtulo says:

  wanaichi ndio sisi katiba itakayo pitishwa ndiyo itakayo tulinda watanzania tuiheshimu katiba kabla hatujaifayia kaz ya kuhidhinisha tuwe makin kuijenga.

 47. Je, una kukopa mengi ya kweli kuangalia kwa? Viwango vya riba nafuu katika mwaka ujao? Ndani ya siku 2-3 kwa kuwa kumbukumbu kuendelea kukataliwa na benki na taasisi za fedha kutoka kwenu? Nzuri! Sisi wote ni aina tofauti za mikopo, kiasi cha chini ya $ 30,000,000.00 $ 50,000.00 kwa upeo wa 2% kila mwaka kiwango cha riba kwa ajili ya biashara ya maendeleo / upanuzi wa biashara na makali ya ushindani. Sisi kuthibitisha, kuaminika, kuaminika, ufanisi, haraka na nguvu. Na mali ubia halisi na aina zote za fedha biashara, jibu la barua pepe hii: clarkfinanceplc11@gmail.com makampuni ya mikopo.

  Sisi kutoa mikopo ya muda mrefu kutoka mwezi mmoja kwa miaka mitano.

  Tunatoa aina zifuatazo za mikopo na wengi zaidi;

  * Mikopo Binafsi (unsecured mikopo)

  * Biashara Mikopo (unsecured mikopo)

  * Pato la mikopo ya mikopo ya jumla *

  * Kuboresha Ukurasa

  Tafadhali, kama wewe ni furaha na nia ya pendekezo yetu ya fedha, usisite kuwasiliana nasi leo, unaweza barua pepe yetu katika barua pepe: clarkfinanceplc11@gmail.com.

  Kwa heshima ya dhati
  Madeni matangazo (baba Bush NAT).

 48. hodi ni wewe katika haraka haja mkopo kulipia kuanza yako madeni ya kuanzisha biashara au nyumba ??? Kisha inakuja teksi kampuni una imani na relay juu ya 100% uhakika sababu hii ni kampuni ambapo i cashed mkopo wangu kwa mama yangu Stella dawa leo ili kuwasiliana na René Mikopo Firm halisi kupimwa na kuaminiwa na leo mimi nina furaha i got mkopo wangu wa $ 120,000 leo ili kupata kushikamana leo mrsstellareneloanfirm@hotmail.com} {barua pepe hapa chini na kupata jibu la matatizo yako yote kwa sababu Siwezi Kunyamaza ushuhuda huu mkubwa peke yangu binafsi ili i aliamua kuandika kwenye tovuti kwa sababu kula furaha kubwa kwa yangu moyo na leo mimi nina kuishi maisha mapya shukrani kwa wote Stella René

  kolochatechee

 49. Mr John Terry says:

  Je, wewe nia ya kupata aina yoyote ya mkopo, kisha kuwasiliana na sisi leo juu ya kupitia: diamondfinancialservice@outlook.com

  Fomu ya Maombi mkopo ..

  Majina kamili:
  jinsia:
  Nchi:
  mji:
  kazi:
  Mapato ya kila mwezi:
  Mkopo Kiasi Inahitajika:
  Mkopo Muda:
  Namba ya simu ya mkononi:
  Mr John Terry
  © 2015 Microsoft Majira faragha & kuki Waendelezaji English (United Kingdom)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>