MTAZAMO WA VIJANA 2010

AJENDA YA VIJANA 2010
Utangulizi
Ajenda ya vijana 2010 ni ilani mbadala ya uchaguzi ya
vijana wa Tanzania inayoainisha vipaumbele kwenye
maeneo 10 ambayo ni nyeti na muhimu kwa manufaa
ya vijana, uhai na mustakabali wa taifa letu Tanzania.
Kabla ya uchaguzi mkuu 2010 ilani hii huwasilishwa
kwa vyama mbalimbali vya siasa vinavyoshiriki zoezi
la uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani
ikiwa kama madai ya vijana wa Tanzania yanayotakiwa
kutekelezwa na serikali ya chama kitakachoshinda
uchaguzi mkuu, kushika dola na kuunda serikali.

1.1 Wadau wa ajenda hii
Harakati za ajenda hii ya vijana zilianza mwaka 2005
na kuwasilishwa kwenye vyama vya siasa vilivyoshiriki
uchaguzi mkuu mwaka 2005. Ajenda ya vijana 2010
imeandaliwa na wadau wa makundi na asasi mbalimbali
za vijana bila kujali itikadi za kidini, rangi, kabila wala
vyama vya siasa chini ya uratibu na usimamizi makini
wa asasi ya Tanzania Youth Vision Association (TYVA).
Madai ya ajenda hii hutokana na uchambuzi yakinifu
wa hali halisi ya maisha ya vijana na Taifa kwa ujumla
kulingana na viashiria vya maendeleo mfano kupungua
kwa vifo, ajira, kilimo n.k vilivyoainishwa katika mipango
mbalimbali ya kitaifa kama MKUKUTA na mikakati
mingine ya ki-sera.

1.2 Malengo ya Ajenda ya Vijana

Kwa kuzingatia historia ya Taifa letu tangu tupate
uhuru kwa zaidi ya miaka 48 iliyopita, hali halisi ya
maisha ya Watanzania kwa pato la taifa na pato la
mtu binafsi imeendelea kuwa uduni. Uduni wa maisha
ya Watanzania umedorora hasa katika upatikanaji
huduma bora za kijamii. Kwa kuzingatia hali ya ulinzi
na usalama wa Taifa na ukweli kuwa vijana hufanya
sehemu kubwa ya watu wote nchini zaidi ya asilimia 30
ambayo ukiunganisha na watoto ni nusu ya Watanzania
wote. Pia kwa kuzingatia kuwa vijana hufanya zaidi ya
asilimia 65 ya nguvu kazi ya Taifa ambayo hata hivyo
Taifa halijaitumia ipasavyo. Ukizingatia kuwa asilimia
kubwa ya wapiga kura mijini na vijijni ni vijana; ilani ya
vijana 2010 ambayo ndiyo ajenda ya maendeleo kwa
vijana na mbadala wa ilani za vyama vya siasa katika
mambo yahusuyo vijana kwa manufaa ya watu wote
hapa nchini imebainisha malengo 10 yenye jumla ya
shabaha 33 ambazo zinatekelezeka endapo serikali
itakayokuwa madarakani baada ya uchaguzi itaamua
kufanya hivyo. Aidha kila shabaha ina malengo madogo
ambayo ndio madai yanayotarajiwa yatekelezwe na
serikali itakayoundwa baada ya Uchaguzi Mkuu 2010.
Malengo kumi ya ajenda ya vijana 2010 ni kama ifuatavyo.
Lengo la kwanza la madai ya vijana ni uanzishwaji wa
baraza huru la Taifa la Vijana na utekelezwaji wa sera ya
vijana. Lengo la pili la madai ya vijana ni ongezeko la ajira
kwa vijana na uboreshwaji wa mazingira ya kazi. Lengo
la tatu ni kuidai serikali iboreshe utoaji wa elimu bora
na kuwezesha mabadiliko ya mfumo wa elimu. Lengo
la nne vijana tunadai ongezeko la ushiriki wa vijana
katika vyombo vya maamuzi na michakato mbalimbali
ya kitaifa na kimataifa.
Lengo la tano tunaidai serikali kuchochea maendeleo
ya michezo na utamaduni wa Tanzania kuanzia ngazi
ya wilaya. Lengo la sita tunaidai serikali iboreshe na
kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa vijana.
Lengo la saba ni kuitaka serikali Kujenga utawala bora
na uwajibikaji. Lengo la nane tunaitaka serikali itakayo
hakikisha umasikini unapungua, na kipato cha kila
kaya kinapanda. Katika lengo la tisa tunaitaka serikali
itakayoweza kuboresha ustawi wa vijana wenye
ulemavu. Lengo la kumi tunaitaka serikali kuwa na sera
ya kimataifa yenye ufanisi na kuhusisha jamii kwa upana
wake.

2.0 Madai ya vijana kwa wagombea,
vyama vya siasa na serikali itakayoshinda
uchaguzi 2010

Madai ya vipaumbele vya vijana kwa wagombea,
vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu 2010
na kutarajia kushinda na kuunda serikali havina budi
kuitilia maanani ajenda hii ya vijana 2010. Madai haya
ni kama ifuatavyo;‐

2.1 Baraza Huru la Vijana la Taifa
• Kuzileta pamoja asasi za vijana, wizara husika
ya vijana na vijana kwa ujumla kuwezesha
uundwaji wa Baraza huru la Taifa la Vijana
ifikapo Januari 2012.
• Kuwezesha utekelezaji wa sera ya maendeleo
ya vijana nchini.

2.2 Ajira
• Kuchochea ongezeko la fursa za ajira binafsi
kwa wakulima wadogo wa kilimo cha kibiashara
katika maeneo ya vijijini.
• Kuongeza tija katika kilimo kiuzalishaji na
kuboresha mazingira ya kazi ya kilimo kwa
wakulima wadogo katika maeneo ya vijijini
• Kuongeza utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali
miongoni mwa vijana wanaojishughulisha na
biashara na fani za kila aina katika wilaya zote
nchi nzima
• Kuwajengea uwezo wa kiushindani vijana
wajasiriamali na kupanua mitaji ya biashara na
kazi zao
• Kutumia nguvu kazi ya Taifa kuongeza fursa za
ajira katika sekta ya umma na sekta binafsi
• Kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi
katika sekta ya umma na sekta binafsi.

2.3 Elimu
• Kupanua upati kanaji wa elimu bora kwa vijana
kwenye shule za msingi na sekondari kati ka
maeneo ya mijini na vijijini
• Kuimarisha ubora na upati kanaji wa elimu ya
juu kwa vijana wote nchini.
2.4 Ushiriki wa Vijana
• Ongezeko la idadi ya vijana kati ka bunge na
mabaraza ya madiwani kuanzia uchaguzi mkuu
2010 na ule wa 2015
• Kuchochea ongezeko la ushiriki wa vijana kati ka
serikali za mitaa kwa ngazi zote
• Kuwezesha uanzishwaji wa programu ya
maendeleo ya kimataifa ya vijana itakayo
husisha taasisi/asasi na vikundi mbalimbali
vya vijana kati ka michakato mbalimbali ya
kimataifa.
• Kuwa na njia imara na mahsusi ya kukusanya
maoni ya vijana kati ka michakato mbalimbali ya
kitaifa mathalani kupiti a taasisi/asasi za vijana
2.5 Michezo na Utamaduni
• Uboreshwaji wa miundombinu ya michezo na
kuhamasisha utamaduni wa Tanzania kuanzia
ngazi ya wilaya
• Uboreshwaji wa utawala wa mamlaka husika
zinazosimamia kazi za sanaa na haki miliki
• Kukuza na kuimarisha mazingira ya matumizi
bora ya vipaji mbalimbali vya vijana kama

2.6 Afya kwa Vijana
• Uboreshwaji wa utoaji wa huduma za afya ya
uzazi kwa vijana kati ka maeneo ya mijini na
vijijini na kuweka msisiti zo maalumu kwenye
kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya
Ukimwi.
• Uboreshwaji wa utoaji wa huduma za msingi za
afya zilizo bora kwa watu wote
2.7 Utawala Bora na Uwajibikaji
• Kuweka sheria “power of recall” itakayo
wawajibisha viongozi wa kisiasa wasiowajibika
kati ka majukumu yao ipasavyo
• Kuwekwa mazingira mazuri yatakayowezesha
uwepo wa kisheria wa mgombea binafsi.
• Umri wa mgombea wa nafasi ya Urais
upunguzwe hadi kufi kia miaka 35
• Kuongeza na kuimarisha uhuru wa vyombo vya
habari
• Kuboresha ufanisi na uwajibikaji wa taasisi
zinazosimamia utawala bora na uwajibikaji
mathalani Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Tume ya Maadili ya viongozi wa
umma, na TAKUKURU
• Maandalizi ya kati ba mpya itayohusisha mahitaji
na matakwa ya makundi yote ya kijamii
2.8 Uchumi wa mtu mmoja mmoja
• Kuhakikisha umasikini unapungua na
kuwawezesha Watanzania kumiliki uchumi
wao.
2.9 Vijana wenye ulemavu
• Kuboresha Utoaji wa Elimu bora kwa Vijana na
watoto wenye Ulemavu
• Kuchukua hatua za makusudi kutekeleza
mkataba wa kimataifa wa watu wenye ulemavu
ili kuboresha ustawi wao kijamii.
• Kuongeza ushiriki wa vijana wenye ulemavu
kati ka vyombo vya maamuzi.
• Kuchochea ongezeko la idadi ya fursa za ajira,
serikalini kwenye sekta binafsi na ajira binafsi
kwa vijana wenye Ulemavu.
• Kuongeza utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali
miongoni mwa vijana wenye ulemavu
wanaojishughulisha na biashara na fani
mbalimbali kati ka wilaya zote nchini
• Kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi
wenye ulemavu mathalani uwepo wa mazingira
rafi ki ya kimiundo mbinu na kupandishwa
vyeo.
• Kuhakikisha uwepo wa mazingira rafi ki ya
kuwawezesha kushiriki ipasavyo kati ka chaguzi
zote nchini.

2.10 Diplomasia
• Kuongeza uwezo wa ushawishi wa nchi kati ka
michakato mbalimbali ya kimataifa.
• Kuboresha ushiriki wa asasi za kiraia hususani
za vijana kati ka maamuzi yanayofanywa na
serikali kati ka michakato ya kimataifa.

MCHAKATO HUU ULIWAHUSISHA WADAU WAFUATAO:
United Nations Association
Chama cha Walemavu Tanzania
Tanzania Youth Vision Association
Philosophy Association of Tanzania
Jukwaa la Vijana TanzaniaDo you like TYVA? You can be a part of this awesome Community


TYVA CONTACTS

OUR MISSION

TYVA is dedicated toward promoting empowerment and self realization of young people through mounting awareness raising, capacity building and networking programs which are youth centered, gender sensitive environmental friendly and readily accessible to vulnerable youth. This is through trainings, Youth dialogues, seminars and workshops.

OUR VISION

To see a free, just, democratic and peaceful society, in which there is active and effective youth participation. .

Follow us on Twitter

@TYVAVijana

- 1 day ago

Aksanteni WanaUnguja kwa ushirikiano wenu , hakika ni mengi tumefahamishana, mpaka wakati mwingine! @DiraYaVijanaTz… https://t.co/hZpULUh23s
h J R