Blog

#BintiJitambue yawafikia Mabinti Mwenge, Vingunguti, Sinza na Arusha

#BintiJitambue, imefanikiwa kukutana na wazazi wa mtaa wa Mlalakua -Mwenge na Kuzungumza nao mambo mengi yanayohusu Afya ya Uzazi, Makuzi na Kujitambua.Kitu kikubwa kilichotufurahisha kutoka kwao, wazazi walituahidi kuwa wazi kwa mabinti zao pindi tu wanapoingia Balehe. Hii isiishie kwao tu bali ni jukumu la wazazi na jamii kwa ujumla. Tunawatakia utekelezaji mwema, katika kufanikisha ndoto za mabinti wote zinatamia. Pia  Team ya Binti Jitambue ilipata nafasi ya kuzungumza na mabinti wa Chakuwama Orphanage Center kilichopo Sinza…Na kuzungumza nao kuhusu kujitambua, makuzi na pia ilitoa mafunzo juu ya umuhimu wa kujiamini na kujithamini kama msichana ili kuweza kufikia malengo kiujumla. Team ya BintiJitambue pia ilipata nafasi ya kutembelea kituo cha Mwana Orphanage Centre kilichopo Vingunguti na kuongea na mabinti waliopo katika kituo hicho juu ya makuzi na kujitambua ili waweze kujithamini, kujiamini na kufikia ndoto zao.

Jijini Arusha,

Walitembelea kituo cha mtoto Compassion kilichopo ndani ya kabisa la Moravian, lililopo Mianzini, siku ya Jumamosi, tarehe 2/7/2016. Kwa lengo la kuwapa mabinti elimu ya uzazi, na kujitambua. Ambapo walifanikiwa kuelimisha mabinti 11 na kutia mkazo kwenye mambo ya ukuaji, usafi, kujithamini na kujiamini kama mabinti na kuwapa motisha ya kujitambua kuwa wao ni hazina kubwa kwa Taifa kiujumla na kwa familia zako za sasa na za baadae. Walipata nafasi ya kusikia changamoto mbali mbali wanazopitia na kuwapa ushauri namna ya kukabiliana na changamoto hizo ili waweze kuwa katika hali salama. Mwisho kabisa tulipata nafasi ya kuwauliza maswali ili kutadhmini uelewa wao juu ya maada na ujumbe tuliofikisha kwao,walijibu vzuri zaidi na kuonesha mabadiliko, kwakujibu katika hali ya kujiamini zaidi na Uhuru zaidi.

#BintiJitambue #GirlsSupportGirls


Leave a Reply


Do you like TYVA? You can be a part of this awesome Community


TYVA CONTACTS

OUR MISSION

TYVA is dedicated toward promoting empowerment and self realization of young people through mounting awareness raising, capacity building and networking programs which are youth centered, gender sensitive environmental friendly and readily accessible to vulnerable youth. This is through trainings, Youth dialogues, seminars and workshops.

OUR VISION

To see a free, just, democratic and peaceful society, in which there is active and effective youth participation.

Follow us on Twitter

@TYVAVijana

- 22 days ago

Ndugu @makwitamakwita1 Mwenyekiti Wa Asasi ya vijana @TYVAvijana akieleza juu ya Dhana ya uwajibikaji #Faya https://t.co/R3x4weP6tM
h J R
@TYVAVijana

- 22 days ago

Taasisi ya Vijana @TYVAvijana kwa kushirikiana na @YUNA_Tz wameandaa mkutano na kujadili kuhusu Uwajibikaji katika… https://t.co/Zkkj3xrjUl
h J R